Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Yesu akamjibu, “Hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa na Mungu. Kwa sababu hiyo, yule aliyenikabidhi kwako ana dhambi kubwa zaidi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Yesu akamjibu, “Hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa na Mungu. Kwa sababu hiyo, yule aliyenikabidhi kwako ana dhambi kubwa zaidi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Yesu akamjibu, “Hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa na Mungu. Kwa sababu hiyo, yule aliyenikabidhi kwako ana dhambi kubwa zaidi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndipo Isa akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndipo Isa akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.”

Tazama sura Nakili




Yohana 19:11
37 Marejeleo ya Msalaba  

Marra kuhani mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru: tuna haja gani ya mashahidi wengine? Sasa mmesikia kufuru yake:


wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa liwali Pontio Pilato.


Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akisema, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni, mehukueni salama.


Killa siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono; lakini saa yenu hii, na mamlaka ya giza.


wakamchukua kwa Anna kwanza: maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule.


Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha.


Bassi Pilato akamwambia, Husemi na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukusulibisha na nina mamlaka ya kukufungua?


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


Bassi wakatafuta kumkamata: lakini hapana aliyenyosha mkono wake illi kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.


Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema Twaona; bassi dhambi yenu inakaa.


mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:


Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.


illi wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


KILLA nafsi itumikie mamlaka makuu; kwa maana hapana mamlaka yasiyotoka kwa Mungu: na mamlaka yaliyopo yameamriwa na Mungu.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Bassi yeye ajuae kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyu ni dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo