Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 18:38 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

38 Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani? Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?” Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyote kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?” Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyote kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?” Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyote kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Pilato akamuuliza Isa, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena, akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Isa, “Sioni msingi wowote wa kumshtaki mtu huyu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Pilato akamuuliza Isa, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Isa, “Sioni kosa lolote alilotenda mtu huyu.

Tazama sura Nakili




Yohana 18:38
14 Marejeleo ya Msalaba  

Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.


Pilato akawaambia, Kwani, ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulihishe.


Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu.


Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?


Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake.


Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake.


Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo