Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 18:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Isa akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni: ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Isa akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 18:37
26 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


Yesu akasimama mbele ya liwali: liwali akamwuliza, akinena, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wanena.


Yesu akasema, Mimi ndio yeye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbingu.


Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajihu, akamwambia, wewe unasema.


Wakasema wote, Bassi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mnasema kama mimi ndiye.


Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Unasema wewe.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoshuhudia, wala hapana anaeukubali ushuhuda wake.


Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.


Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako.


Nami, kwa sababu naisema kweli, hamniamini.


Nani wenu anishuhudiae kuwa nina dhambi? Nikisema kweli, mbona ninyi hamniamini?


Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli.


Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti.


Hivi tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, na mbele zake tutatuliza mioyo yetu


Sisi twatokana na Mungu. Yeye anijuae Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Hivi twaijua Roho ya kweli, na roho ya upotevu.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo