Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 18:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa unajisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa unajisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa unajisi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Ndipo viongozi wa Wayahudi wakamchukua Isa kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala Mrumi. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri. Ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani ya jumba kwa sababu walitaka kushiriki katika Pasaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Ndipo Wayahudi wakamchukua Isa kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka.

Tazama sura Nakili




Yohana 18:28
33 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya praitorio, wakamkusanyia kikosi kizima.


Askari wakamchukua ndani ya sebule, ndiyo Praitorio, wakakusanya pamoja kikosi kizima.


Hatta ulipokuwa mchana wakakusanyika jamii ya wazee wa watu, na makuhani wakuu, na waandishi, wakamleta kwa haraza yao, wakisema,


Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; wengi wakapanda toka inchi yote pia kwenda Yerusalemi kabla ya Pasaka, illi wajitakase.


wakamchukua kwa Anna kwanza: maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule.


Simon Petro akamfuata Yesu, na mwanafunzi mwingine: na yule mwanafunzi alikuwa anajulika na kuhani mkuu: akaingia pamoja na Yesu behewani mwa kuhani mkuu; lakini Petro akasimama nje mlangoni.


Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?


Lakini kwenu kuna desturi, ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka: bassi, wapenda niwafungulie mfalme wa Wayahudi?


Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.


Ilikuwa Maandalio ya Pasaka: ilikuwa panapo saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, mfalme wenu!


akaingia tena Praitorio, akamwamhia Yesu, Umetoka wapi wewe? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote.


Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis.


Bassi, tuma watu kwenda Yoppa, ukamwite Simon aitwae Petro, aje hapa; anakaa katika nyumha ya Simon, mtengenezaji wa ngozi, karibu ya pwani: nae akija atasema nawe.


Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.


Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo