Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 18:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Isa akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni, mahali Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Isa akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni, mahali ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri.

Tazama sura Nakili




Yohana 18:20
25 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi wakiwaamhieni, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.


Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata.


Marra kuhani mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru: tuna haja gani ya mashahidi wengine? Sasa mmesikia kufuru yake:


Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.


Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.


Petro akamchukua akaanza kumkemea.


Bassi killa siku alikuwa akifundisha hekaluni wakati wa mchana; na wakati wa usiku akitoka, na kulala katika mlima uitwao mlima wa mizeituni.


Nae alikuwa akifundisha katika masunagogi yao, akitukuzwa na watu wote.


Ya nini kumuliza? waulize wale waliosikia, ni nini niliyosema nao: wao wanajua niliyowaambia.


Maneno haya aliyasema sunagogini, alipokuwa akifundisha huko Kapenaum.


Hatta ilipokuwa katikati ya siku kuu Yesu akapanda, akaingia hekalui akafundisha.


Na kumbe! ananena waziwazi wala hawamwambii neno? Yumkini wakuhwa wanajua kwa hakika ya kuwa huyu ni Kristo!


Bassi Yesu akapaaza sauti yake hekaluni, akifundisha, akisema, Mimi mnanijua, na nitokako mnakujua; wala sikuja kwa naisi yangu, illa yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi.


Kwa maana hakuna mtu afanyae neno kwa siri, na yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya haya, jidhihirishe kwa ulimwengu.


Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha.


Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.


Kwa maana mfalme anajua khabari za mambo haya, na naweza kusema nae bila khofu, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo