Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 18:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Bassi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga wako alani mwake. Kikombe alichonipa Baba, nisikinywee?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Isa akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Isa akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba?”

Tazama sura Nakili




Yohana 18:11
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomha. Mwaweza kuuywea kikombe nitakachonywea mimi, na kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza.


Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.


Maana mataifa wa dunia huyatafuta hayo yote, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.


Baba, ukipenda, uniondolee kikombe hiki: lakini si kama nitakavyo mimi, illa utakavyo wewe vifanyike.


Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu: watumishi wangu wangalinipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa.


Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.


maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;


katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo