Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 17:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale ulionipa, maana ni wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale ulionipa, maana ni wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale ulionipa, maana ni wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Ninawaombea wao. Mimi siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako.

Tazama sura Nakili




Yohana 17:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.


Wachungaji walipoona, wakakimbia, wakaenda zao wakaeneza khabari mjini na mashambani.


Na mimi nitamwomba Baba, nae atawapa Mfariji mwingine, akaae nanyi hatta milele,


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele.


Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao walakaoniammi kwa sababu ya neno lao.


Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho.


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo