Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 17:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Na uhai wa milele ndio huu: Kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Na uhai wa milele ndio huu: Kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Na uhai wa milele ndio huu: kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mwenyezi Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.

Tazama sura Nakili




Yohana 17:3
52 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.


akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.


je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?


Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni.


Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?


Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu.


Lakini mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, nae ndiye aliyenituma.


Bassi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngaliuijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.


Erevukeui kama ipasavyo, wala insiteude dhambi; kwa maana wengine hawamfahamu Mungu. Ninasema haya niwafedheheshe.


Bassi, kwa khabari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hapana Mungu mwingine illa mmoja tu.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,


katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu;


kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe;


Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.


(na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


Killa anikanae Mwana, amkana Baba pia.


Sisi twatokana na Mungu. Yeye anijuae Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Hivi twaijua Roho ya kweli, na roho ya upotevu.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo