Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 17:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Nimefanya jina lako lijulikane kwao, nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao, na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili kwamba upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”

Tazama sura Nakili




Yohana 17:26
28 Marejeleo ya Msalaba  

Katika siku ile mtajua ninyi, ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, na ninyi ndani yangu, na mimi ndani yenu.


Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.


Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni.


Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu.


Kama Baba alivyonipenda mimi, nami nimewapenda ninyi; kaeni katika pendo langu.


mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.


Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu, na mimi ndani yake.


Nami siutafuti ntukufu wangu; yuko atafutae na kuhukumu.


Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu u katika hali ya kufa kwa sababu ya dhambi, bali roho yenu i katika hali ya uzima, kwa sababu ya haki.


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Maana kama vile mwili ni mmoja, nao nna viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule mmoja, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


Kristo akae mioyoni mwemi kwa imani; illi ninyi, mkiwa na mizizi na misingi katika upendo,


kwa kuwa tu viungo vya mwili wake, na nyama yake, na mifupa yake.


Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa.


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi vote na mamlaka.


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


akinena, Nitalikhubiri jina lako kwa ndugu zangu; kati kati ya kanisa nitakuimba,


Nae azishikae amri zake hukaa ndani yake, nae ndani yake. Na hivi tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa Roho aliyotupa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo