Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 17:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako. Wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma mimi.

Tazama sura Nakili




Yohana 17:21
37 Marejeleo ya Msalaba  

Na ufalme nkilitinika juu ya nafsi yake ufalme ule hauwezi kusimama;


Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.


Mimi na Baba yangu tu nmoja.


lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujua na kuamini ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.


Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Mungu akiwa ametukuzwa ndani yake, Mungu nae atamtukuza ndani ya nafsi yake; na marra atamtukuza.


Hivi watu wote watajua ya kuwa m wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.


Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi.


Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni.


Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao walakaoniammi kwa sababu ya neno lao.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.


vivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na sisi sote tu viungo killa mmoja kwa wenzake.


Nawasihi ninyi, ndugu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnene nyote mamoja, pasiwe kwenu faraka, bali mwe mmekhitimu katika nia moja na shauri moja.


Maana kama vile mwili ni mmoja, nao nna viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule mmoja, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.


Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja nae.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


Kwa maana watatu ni mashahidi mbinguni, Baba, Neno, na Robo Mtakatifu, ua watatu hawa ni umoja.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo