Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 17:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.

Tazama sura Nakili

Yohana 17:12
17 Marejeleo ya Msalaba  

Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.

Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.

illi litimizwe lile neno alilolisema, Hawa ulionipa sikupoteza hatta mmoja wao.

Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.

atwae sehemu yake ya khuduma hii na utume huu, alioukosa Yuda aende zake mahali pake.

Kwa hiyo tena Mungu akamtukuza mno, akamkarimia Jina lile lipitalo killa jina;

Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,

na tena, Nitamtumaini: na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.

Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

Na macho yake yalikuwa kama mwako wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi, nae ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu illa yeye mwenyewe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo