Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 16:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini, nawaambieni ukweli: Afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini, nawaambieni ukweli: Afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini, nawaambieni ukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; lakini nikienda nitamtuma kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, lakini nikienda nitamtuma kwenu.

Tazama sura Nakili




Yohana 16:7
19 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu.


Lakini kwa kweli nawaambieni, Palikuwa wajane wengi katika Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita; njaa kuu ikaingia inchi yote:


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataionja mauti kabisa hatta watakapouona ufalme wa Mungu.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Nakwenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi, kwa sababu nashika njia kwenda kwa Baba: kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.


Bassi nikishika njia kwenda kuwaandalia mahali, nitakuja tena, niwakaribisheni kwangu; illi nilipo mimi, nanyi mwepo.


Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia.


Na akiisha kuja yeye, atauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi, na haki, na hukumu;


Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa.


Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.


Maana mateso mepesi yetu, yaliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele ulio mwingi sana zaidi;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo