Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 16:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Yohana 16:30
12 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi baadhi ya wanafunzi wake walisemezana, Neno gani hili analosema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo na mtaniona? na, Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba?

Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni.

Katika siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba;

Yesu akawajihu, Sasa hivi mnaamini?

kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.

Mwanzo huu wa ishara Yesu alifanya Kana ya Galilaya, akauonyesha utukufu wake, wanafunzi wake wakamwamini.

Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.

Maana Baba ampenda Mwana, amwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; na kazi kubwa zaidi kuliko hizi atamwonyesha illi ninyi mpate kustaajabu.

Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.

Wala hakuna kiumbe kisicho wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu, na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo