Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 16:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Katika siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Siku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Siku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu,

Tazama sura Nakili




Yohana 16:26
9 Marejeleo ya Msalaba  

Na mimi nitamwomba Baba, nae atawapa Mfariji mwingine, akaae nanyi hatta milele,


Katika siku ile mtajua ninyi, ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, na ninyi ndani yangu, na mimi ndani yenu.


Yesu alifahamu ya kwamba walitaka kumwuliza akawaambia, Hili ndilo mnalotafuta ninyi kwa ninyi, ya kuwa nalisema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na bado kitambo na mtaniona?


Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni.


Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu.


Na kwa ajili yao najitakasa, illi na hawa watakaswe katika kweli.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako.


Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo