Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 16:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mtalia, na kuomboleza, bali, ulimwengu utafurahi: ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Nawaambieni kweli, nyinyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi; mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Nawaambieni kweli, nyinyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi; mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Nawaambieni kweli, nyinyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi; mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.

Tazama sura Nakili




Yohana 16:20
44 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.


Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika.


Jogoo akawika marra ya pili. Petro akalikumbuka neno lile aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo marra mbili, utanikana marra tatu. Na alipolifikiri, akalia.


Huyu akashika njia akawapa khabari wale waliokuwa pamoja nae tangu zamani, wangali wakiomboleza na kulia.


Alipoondoka katika kuomba, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala kwa huzuni, akawaambia,


Akatoka nje, akalia kwa uchungu.


Wakamfuata makutano mengi ya watu, na ya wanawake, waliojipigapiga, wakaomboleza.


Akawaambia, Maneno gani haya mnayobishana katika kutembea kwenu? na tena nyuso zenu zimekunjamana.


nasi twalitaraja ya kuwa yeye ndiye atakaekomboa Israeli. Hatta pamoja na haya yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipokuwa haya.


M kheri ninyi mnaoona njaa sasa: kwa subabu mtashiba. M kheri ninyi mliao sasa: kwa sababu mtacheka.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Illa kwa sababa nimewaambieni haya, huzimi imejaa mioyoni mwenu.


Akiisha kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Bassi wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


Wala si hivyo tu, illa na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambae kwa yeye tuliupokea upatanisho.


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,


Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Nao wakaao juu ya inchi watafanya furaha juu yao ua kushangilia. Na watapelekeana zawadi kwa kuwa manabii hawo wawili waliwatesa wao wakaao juu ya inchi.


Kwa kadiri aliyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa alisema moyoni mwake, Nimeketi malkiya, nami si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo