Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 16:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Yesu alifahamu ya kwamba walitaka kumwuliza akawaambia, Hili ndilo mnalotafuta ninyi kwa ninyi, ya kuwa nalisema, Bado kitambo nanyi hamnioni, na bado kitambo na mtaniona?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, “Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, “Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, “Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Isa akatambua kuwa walitaka kumuuliza kuhusu hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Isa akatambua kuwa walitaka kumuuliza juu ya hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona?’

Tazama sura Nakili




Yohana 16:19
18 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi msifanane na hawo; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.


Nae Yesu, akijua mawazo yao, akasema, Jinsi gani mnawaza maovu mioyoni mwenu?


Nao hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.


Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi.


Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi.


Bado kitambo, nanyi hamnioni tena; na bado tena kitambo, na mtaniona. Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba.


Bassi walisema. Neno gani hili analosema, hili Bado kitambo? Hatujui asemalo.


Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni.


Katika siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea Baba;


Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu.


Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.


Yesu akajua nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanaliumigʼunikia neno hili, akawaambia, Neno hili linawachukiza?


Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.


Wala hakuna kiumbe kisicho wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu, na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo