Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 16:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Bado kitambo, nanyi hamnioni tena; na bado tena kitambo, na mtaniona. Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Isa akaendelea kusema, “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.”

Tazama sura Nakili




Yohana 16:16
19 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.


bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu,


Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi.


kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;


Bassi na ninyi sasa hivi mna huzuni; lakini nitawaona tena, na moyo wenu utafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleae.


Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba.


Lakini sasa nakwenda zangu kwake aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizae, Unakwenda zako wapi?


Na sasa naja kwako; na haya nayasema ulimwenguni, illi wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.


Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu.


Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.


na baada ya kuteswa kwake, akawadhihirisbia ya kwamba yu hayi, kwa dalili nyingi, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyonkhusu ufalme wa Mungu.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo