Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 16:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonesha mambo yajayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.

Tazama sura Nakili




Yohana 16:13
32 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.


Roho ya kweli; ambae ulimwengu hauwezi kumkubali, kwa kuwa haumwoni wala haumjui: bali ninyi mnamjua; maana anakaa kwenu, nae atakuwa ndani yenu.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia.


Hatta ninayo mengi bado ya kuwaambieni, lakini hamwezi kuyastahimili sasa.


Aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoshuhudia, wala hapana anaeukubali ushuhuda wake.


Niliyoyaona kwa Baba yangu udiyo niyanenayo: nanyi vivyo hivyo mliyoyaona kwa baba yenu, ndiyo myatendayo.


Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.


illa ya kuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na mateso yaningoja.


Usiogope, Paolo, huna buddi kusimama mbele ya Kaisari: tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.


illi wahukumiwe wote wasioamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.


Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,


KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,


Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.


Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.


Sisi twatokana na Mungu. Yeye anijuae Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Hivi twaijua Roho ya kweli, na roho ya upotevu.


Huyu ndiye ajae kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Na Roho ndiyo ishuhuduyo, kwa sababu Roho ndiyo iliyo kweli.


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Bassi, yaandike mambo uliyoyaona, nayo yatakayokuwa baada ya hayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo