Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 15:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, mtaomba killa mtakalo, na mtafanyiziwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa.

Tazama sura Nakili




Yohana 15:7
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ombeni na mtapewa; tafuteni na mtaona; bisheni na mtafunguliwa:


Na mkiomba lo lote kwa jina langu, hili nitalifanya, Baba atukuzwe ndani ya Mwana.


Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.


Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni.


Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli;


Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.


bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hatta muhulla uliokwisha kuamriwa na baba.


Nasema, Enendeni kwa Roho, nanyi hamtatimiza tamaa za mwili.


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.


Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.


na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.


Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo