Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 15:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Mimi mzabibu; ninyi matawi; akaae ndani yangu, na mimi ndani yake, huyu huzaa Sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.

Tazama sura Nakili




Yohana 15:5
28 Marejeleo ya Msalaba  

lakini hana mizizi udani yake, hukaa muda mchache; ikitukia shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa.


Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.


Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.


Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.


Kama huyu asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno.


Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo.


vivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na sisi sote tu viungo killa mmoja kwa wenzake.


Lakini sasa mkiisha kuandikwa huru, na kuwa mbali ya dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, faida yenu mnayo, ndio kutakaswa, na mwisho wake uzima wa milele.


Kadhalika, ndugu zangu, na ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka, kusudi tumzalie Mungu matunda.


Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule timmegao, si ushirika wa mwili wti Kristo?


Maana kama vile mwili ni mmoja, nao nna viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule mmoja, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.


Na ninyi m mwili wa Kristo, na viungo vya mwili huo, mmoja hiki na mmoja hiki.


Maana hatuwezi kutenda neno kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.


Na yeye amruzukuye mbegu mwenye kupanda, atoae mkate uwe chakula, atawapeni mbegu za kupanda na kuzizidisha, atayaongeza mazao ya haki yenu;


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


(kwa kuwa tunda la nura ni katika wema wote na haki na kweli);


mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.


Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu.


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu;


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo