Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 15:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakanichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakanichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakanichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Kama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine yeyote, hawangekuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii, na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Kama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine yeyote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu.

Tazama sura Nakili




Yohana 15:24
36 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaha walimwamini: nanyi mlipoona, hamkutuhu haada ya haya, na kumwamini.


Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.


Akaondoka marra, akajitwika kitanda chake, akatoka mbele yao wote; hatta wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakinena, Namna hii hatujapata kuyaona kamwe.


Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote;


Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe?


Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;


Makuhani wakuu wakafanya shauri wamwue Lazaro nae;


Nae anitazamae mimi, amtazama yeye aliyenipeleka.


Yesu akamwambia, Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba?


Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka.


Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; sasa hawana udhuru kwa dhamhi yao.


Anichukiae mimi, humchukia na Baba yangu.


Kiva khabari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.


Lakini naliwaambieni ya kwamba mmeniona bila kuniamini.


Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?


Tangu awali haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu aliyezaliwa hali hii.


Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema Twaona; bassi dhambi yenu inakaa.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


watu wti nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakahari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,


makhaini, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko Mungu;


Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo