Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 15:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Kumbukeni niliyowaambieni: Mtumishi si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na nyinyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Kumbukeni niliyowaambieni: Mtumishi si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na nyinyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Kumbukeni niliyowaambieni: mtumishi si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na nyinyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia.

Tazama sura Nakili




Yohana 15:20
22 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumishi hampiti bwana wake.


Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa:


Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;


Mwanafunzi hampiti mwalimu wake; illa killa aliyekhitimu atakuwa sawa na mwalimu wake.


Bassi Wayahudi wakaokota mawe tena, illi wampige.


Na Makuhani na Mafarisayo wametoa amri ya kwamba, mtu akimjua alipo, alete khabari, wapate kumkamata.


Amin, amin, nawaambieni, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake: wala mtume si mkuu kuliko yeye aiiyempeleka.


Kwa sababu hiyo Wayahudi wakaanza kumwudhi Yesu, wakitaka kumwua, kwa kuwa alitenda haya siku ya sabato.


Mafarisayo wakawasikia makutano wakinungʼunika hivi kwa khabari zake: bassi Mafarisayo na makuhani wakuu wakatuma watumishi illi wamkamate.


Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


Bassi wakatwaa mawe wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia;


twatupwa chini, bali hatuangamizwi;


waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;


Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo