Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 15:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Nyinyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita nyinyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Nyinyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita nyinyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Nyinyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita nyinyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya. Bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu.

Tazama sura Nakili




Yohana 15:15
32 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.


Akawageukia wanafunzi wake kwa faragha, akawaambia, Ya kheri macho yatazamayo mnayoyatazama ninyi.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Amin, amin, nawaambieni, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake: wala mtume si mkuu kuliko yeye aiiyempeleka.


Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu.


Hatta ninayo mengi bado ya kuwaambieni, lakini hamwezi kuyastahimili sasa.


Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao.


Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii.


Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.


Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


Maana sijui nifanyalo; kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; na lile nilichukialo nalitenda.


Maana ni nani aliyejua nia ya Bwana, amwelemishe? Lakini sisi tuna nia ya Kristo.


Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.


akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,


ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho;


siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake:


tokea sasa, si kama mtumwa, baii lieha ya mtumwa, ndugu mpendwa, kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana.


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa ni haki: nae aliitwa raliki wa Mungu.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo