Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 15:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Haya nimewaambieni, illi furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu iwe kamili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili.

Tazama sura Nakili




Yohana 15:11
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kamleteni yule ndama aliyenona, mkamchinje: tukale na kufurahi.


Tena kufanya furaha na kuona furaha kulikuwa wajib, kwa maana huyu ndugu yako alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana.


Bassi amwonapo humweka mabegani mwake, akifurahiwa.


Bassi, aionapo, huwaita shoga zake na jirani zake, hunena, Furahini pamoja nami, kwa maana nimeiona ile mpia niliyoipoteza.


Mpaka leo hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, na mtapata, furaha yenu iwe timilifu.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Na sasa naja kwako; na haya nayasema ulimwenguni, illi wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.


Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


Nami nikitumaini haya, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, illi muendelee mkapate kufurahi katika imani;


ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa,


Na haya twawaandikieni, illi furaha yenu itimizwe.


Kwa kuwa nina maneno mengi ya kuwa-andikia, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraja kuja kwenu, na kusema nanyi mdo-mo kwa mdomo, illi furaha yenu itimizwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo