Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 14:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Amani nawaachieni; amani yangu nawatolea; si kama ulimwengu utoavyo, mimi nawatolea. Msifadhaike moyo wenu, wala msiwe na woga.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 “Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 “Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 “Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Tazama sura Nakili




Yohana 14:27
65 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, msiwaogope, kwa maana hakuna jambo lililostirika, ambalo halitafunuliwa baadae; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana baadae.


Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuelekeza miguu yetu mnamo njia ya amani.


Na nyumba yo yote mwingiayo, kwanza neneni, Amani iwe nyumbani humu.


Lakini nawaambia ninyi rafiki zangu, Msiwaogope wao wauuao mwili na baada ya haya hawana neno la kutenda la zaidi.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


MSIFADHAIKE mioyo yenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Ikawa jioni katika siku ile ya kwanza ya sabato, na milango imefungwa walipokuwapo wanafunzi kwa khofu ya Wayahudi, akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani kwenu.


Bassi Yesu akawaambia marra ya pili, Amani kwenu; kama Baba alivyonipeleka, nami nawatuma ninyi.


Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo ndani marra ya pili, na Tomaso pamoja nao. Yesu akaja, milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani kwenu.


Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akikhubiri amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),


Bwana akamwambia Paolo kwa njozi nsiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,


kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.


Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya roho ni uzima na amani.


Neema na iwe kwenu, na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.


Neema iwe kweuu, na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo,


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Na wote watakaoiendea kanuni hii, amani kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.


Na amani va Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.


kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote nae, akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya inchi, au vilivyo mbinguni.


Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.


Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo.


Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani siku zote kwti njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.


Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi.


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


aliyegawiwa na Ibrahimu sehemu ya kumi ya vitu vyote; (kwanza kwa tafsiri, mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemi, maana yake, mfalme wa amani;


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo