Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 14:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Asiyenipenda, hayashiki maneno yangu; na neno mnalolisikia silo langu, bali lake Baba aliyenipeleka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu, na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.

Tazama sura Nakili




Yohana 14:24
19 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.


Huamini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu? Maneno niwaambiayo mimi, sisemi kwa shauri langu tu; lakini Baba akaae ndani yangu huzifanya kazi zake.


Mkinipenda mtazishika amri zangu.


Haya nimewaambia, nikikaa kwenu.


Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.


Na neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hamwamini yeye alivetumwa nae.


Bassi Yesu akawajibu akasema, Elimu yangu siyo yangu, illa yake yeye aliyenipeleka.


Bassi Yesu akapaaza sauti yake hekaluni, akifundisha, akisema, Mimi mnanijua, na nitokako mnakujua; wala sikuja kwa naisi yangu, illa yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi.


Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.


Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.


Niliyoyaona kwa Baba yangu udiyo niyanenayo: nanyi vivyo hivyo mliyoyaona kwa baba yenu, ndiyo myatendayo.


Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo