Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 14:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendae; nae anipendae atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda, na kujidhihirisha kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye. Naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Tazama sura Nakili




Yohana 14:21
43 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika.


Mkinipenda mtazishika amri zangu.


Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.


Ninyi m rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.


Yeye atanitukuza mimi: kwa kuwa atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari.


kwa maana Baba mwenyewe awapenda ninyi, kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, mkaamini ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba.


mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.


nikamwona akiniambia, Hima, toka katika Yerusalemi upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika khabari zangu.


Kwa ajili ya kitu hiki nalimsihi Bwaua marra tatu kinitoke.


Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema na iwe nanyi. Amin.


Lakiui yeye alishikae neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ilivi twajua ya kuwa tumo ndani yake.


FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.


Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kuzisinka amri zake: na amri zake si nzito.


Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Illi ndiyo ile amri, kama ulivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa.


Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake.


Tazama, nasimama mlangoni, nabisha: mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula pamoja nae, na yeye pamoja nami.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo