Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 13:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 “Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 “Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane.

Tazama sura Nakili




Yohana 13:34
38 Marejeleo ya Msalaba  

bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa;


Haya nawaamuru, mpate kupendana.


Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


Peudo halimfanyizii jirani neno baya; bassi pendo ndio utimilifu wa sharia.


Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendae mtu mwenzake ameitimiza sharia.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sharia ya Kristo.


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu;


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


Illakini mkiitimiza sharia ya kifalme kama ilivyoandikwa. Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vyema.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;


Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.


Na amri hii tumepewa nae, ya kwamba yeye ampendae Mungu, ampende na ndugu yake.


Na sasa, Bibi, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo