Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 13:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Na baada ya lile tonge, Shetani akamwingia. Bassi Yesu akamwambia, Uyatendayo, yatende upesi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Yuda alipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia. Basi Yesu akamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanye haraka!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Yuda alipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia. Basi Yesu akamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanye haraka!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Yuda alipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia. Basi Yesu akamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanye haraka!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia. Isa akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda, litende haraka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia. Isa akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda litende haraka.”

Tazama sura Nakili




Yohana 13:27
16 Marejeleo ya Msalaba  

Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.


Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.


Marra akaingia kwa haraka mbele ya mfalme akaomba akinena, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.


Shetani akamwingia Yuda, aitwae Iskariote, nae alikuwa katika hesabu ya wale thenashara.


Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti,


Wala hapana mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu hatta akamwambia hivi.


Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani?


Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo