Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 13:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mmoja wa wanafunzi, ambaye Yesu alikuwa anampenda sana, alikuwa ameketi karibu na Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mmoja wa wanafunzi, ambaye Yesu alikuwa anampenda sana, alikuwa ameketi karibu na Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mmoja wa wanafunzi, ambaye Yesu alikuwa anampenda sana, alikuwa ameketi karibu na Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Mmoja wa wanafunzi wake, ambaye Isa alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Mmoja wa wanafunzi wake ambaye Isa alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Isa.

Tazama sura Nakili




Yohana 13:23
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa maskini akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Akafa na yule tajiri, akazikwa.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Bassi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake, wakisema, Bwana, yeye umpendae hawezi.


Bassi Wayahudi wakanena, Angalieni jinsi alivyompenda.


Nae Yesu alimpenda Martha na dada yake ua Lazaro.


Bassi Simon Petro akampungia mkono huyo, amwulize, Ni nani anaemtaja?


Bassi yeye akimwegamia Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?


Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako.


Bassi akaenda mbio hatta kwa Simon Petro, na kwa mwanafunzi yule mwingine aliyependwa na Yesu, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.


Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye?


Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.


Bassi mwanafunzi yule ambae Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Bassi Simon Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo