Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 13:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni kutimiza andiko lisemalo, ‘Yeye aliyekula chakula changu ameinua kisigino chake dhidi yangu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili Andiko lipate kutimia, kwamba, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’

Tazama sura Nakili




Yohana 13:18
27 Marejeleo ya Msalaba  

na adui wa mtu ndio wale wa nyumbani mwake.


Walipokuwa wakila, akasema, Amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.


Akajibu, akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika sahani, ndiye atakaenisaliti.


Ilipokuwa jioni yuaja pamoja na wathenashara.


Nao wakiisha kuketi chakulani, wakila, Yesu akasema, Amin, nawaambieni, mmoja wenu, nae anakula pamoja nami, atanisaliti.


Akawaamhia, Ni mmoja wa wathenashara, yeye achovyae pamoja nami katikakombe.


Illa angalieni, mkono wake anisalitiye u pamoja nami mezani.


Alipokwisha kusema haya, Yesu akafadhaika rohoni, akashuhudu, akinena, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.


Wanafunzi wakatazamana, wakiona mashaka, ni nani anaemtaja,


Bassi Yesu akajibu, Ni mtu yule nitakaemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akampa Yuda, mwana wa Simon Iskariote.


Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.


Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeyapenda yaliyo yake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua ninyi katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.


Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre.


Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.


illi neno lake Yesu litimizwe, alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa.


Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.


Kwa maana haya yalitukia andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena,


Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.


Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani?


Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,


hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu:


Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.


Wala hakuna kiumbe kisicho wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu, na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo