Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:48 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

48 Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: Neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: Neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Yuko anayehukumu yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

48 Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili




Yohana 12:48
36 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.


Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Hatta andiko hili hamjalisoma? Jiwe walilokataa waashi Hili limekuwa jiwe kuu la pembeni.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.


Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.


Lakini kwanza hana buddi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi biki.


Waliposikia wakasema, Mungu na apishe mbali. Akawakazia macho, akasema, Maana yake nini, bassi, neno hili lililoandikwa, Jiwe walilolikataa waashi Hili limekuwa jiwe kuu la pembeni?


Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae.


Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu.


Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.


Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba: yuko anaewashitaki, yaani Musa, mnaemtumaini ninyi.


Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho.


Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Na itakuwa ya kwamba kilia mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.


katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo.


Ijapokuwa injili yetu imesetirika, imesetirika kwao wanaopotea;


katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;


tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tukionyana; na tukizidi, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,


Lakini mbingu za sasa na inchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hatta siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wana Adamn wasiomcha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo