Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:43 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

43 Kwa maana waliupenda utukufu wa wana Adamu kuliko utukufu wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zinazotoka kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.

Tazama sura Nakili




Yohana 12:43
20 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.


Akasema, Vema, mtumishi mwema, kwa sababu umekuwa mwaminifu kwa kitu kilicho kidogo, bassi, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Sipokei utukufu kwa wana Adamu.


Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?


Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.


Yesu akajibu, Nikijitukuza nafsi yangu, utukufu wangu si kitu; anitukuzae ni Baba yangu; mmnenae ninyi kuwa ni Mungu wenu.


hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Maana mtu mwenye kubaliwa si yeye ajisifuye, hali yeve asifiwae na Bwana.


Hatukutaka kusifiwa na watia Adamu, wala na ninyi, wala na wengine, tulipokuwa tuliweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;


bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo