Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:38 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

38 illi litimizwe lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, nani aliyeziamini khabari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: “Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Mwenyezi Mungu umefunuliwa kwa nani?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Bwana Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Bwana Mwenyezi umefunuliwa kwa nani?”

Tazama sura Nakili




Yohana 12:38
24 Marejeleo ya Msalaba  

Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya katika khabari zenu, akinena,


Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni.


Walipokwisha kumsulibi, wakagawa nguo zake, wakipiga kura: illi litimie neno lililonenwa na nabii. Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.


Lakini ijapokuwa amefanya ishara kubwa namna hii mbele yao, hawakumwamini;


Kwa sababu hii hawakuweza kuamini, kwa sababu Isaya alisema tena,


Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre.


Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.


Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.


Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?


Na Isaya ana ujasiri mwingi, anasema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia.


bali kwao waitwao, Wayahudi na Wayunani pia, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.


alipoona vema kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, illi niwakhubiri mataifa khabari zake, marra sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo