Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Ndipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingali pamoja nanyi. Nendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakoenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Ndipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda.

Tazama sura Nakili




Yohana 12:35
27 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamweleza, Yesu wa Nazareti anapita.


Bali akienda usiku, hujikwaa, kwa sababu nuru haimo ndani yake.


Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.


Maadam mnayo nuru, iaminini nuru, mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake akajificha nao.


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Bado kitambo, nanyi hamnioni tena; na bado tena kitambo, na mtaniona. Kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba.


Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo;


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


Kwa maana zamani mlikuwa giza, bali sasa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo