Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Bassi makutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hatta milele: nawe wanenaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Umati ule wa watu wakapaza sauti, wakasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba Al-Masihi adumu milele; hivyo wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Ule umati wa watu ukapiga kelele, ukasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba ‘Al-Masihi adumu milele.’ Wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”

Tazama sura Nakili




Yohana 12:34
26 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akaenda pande za Kaisaria Filipi, akawauliza wanafunzi wake akinena, Watu huninena mimi, Mwana wa Adamu, kuwa nani?


Hatta alipoingia Yerusalenn, mji wote ukataharuki, nkinena, Ni nani huyu?


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


Yesu akawajibu, Haikuandikwa katika torati yenu, ya kama, Mimi nilisema, Ninyi m miungu?


Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu.


Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre.


Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.


hali yeye, kwa kuwa akaa milele, ana ukuhani usioondoka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo