Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Bassi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, na nitalitukuza tena.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, na nitalitukuza tena.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, na nitalitukuza tena.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, ikasema, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”

Tazama sura Nakili




Yohana 12:28
22 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako.


Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.


na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.


sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwana wangu mpendwa, ndiwe unipendezae.


Akasema, Abba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikomhe hiki: walakini, si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.


Likawako wingu, likawatia uvuli: sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ui Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.


Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.


Sauti ikatoka katika lile wingu ikasema, Huyu ni Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.


Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali kwa ajili ya utukufu wake Mungu, illi Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.


Bassi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga wako alani mwake. Kikombe alichonipa Baba, nisikinywee?


Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe kwake.


illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.


illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni;


kwake yeye utukufu katika Kanisa, na katika Kristo Yesu hatta vizazi vyote vya milele na milele. Amin.


Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, ya kama, Huyu ndiye mwanangu nimpendae, amhae nimependezwa nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo