Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 12:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Sasa roho yangu imefadhaika; niseme nini? Baba, uniokoe na saa hii. Lakini kwa ajili ya hayo naliifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 “Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja – ili nipite katika saa hii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 “Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja – ili nipite katika saa hii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 “Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja — ili nipite katika saa hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii’? Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.

Tazama sura Nakili




Yohana 12:27
24 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako.


Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike.


Khalafu akawaendea wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa hatta mwisho, kapumzikeni: saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dbambi.


Nae kwa kuwa alikuwa na huzuni sana, akazidi kuomba kwa bidii. Hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka hatta inchi.


Killa siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono; lakini saa yenu hii, na mamlaka ya giza.


Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.


Yesu akajibu, akinena, Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu.


Alipokwisha kusema haya, Yesu akafadhaika rohoni, akashuhudu, akinena, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.


Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.


Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo