Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 11:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Ni Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu yake kwa nywele zake, ambae ndugu yake Lazaro alikuwa hawezi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwa mgonjwa).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwa mgonjwa).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwa mgonjwa).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 (Huyu Mariamu, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye alimpaka Bwana Isa mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Huyu Maria, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye yule ambaye alimpaka Bwana Isa mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.

Tazama sura Nakili




Yohana 11:2
11 Marejeleo ya Msalaba  

Nae akiwapo Bethania, nyumbani mwa Simon mwenye ukoma, ameketi chakulani, akaja mwanamke mwenye kibweta cha alabastro cha marhamu ya hali udi, safi, ya thamani nyingi; akakivunja kibweta cha alabastro akaimimina kichwani pake.


Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.


Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine?


Bassi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.


Bassi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake, wakisema, Bwana, yeye umpendae hawezi.


Bassi Mariamu, alipofika pale alipokuwapo Yesu, akamwona, akaanguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungaliwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.


Bassi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akaifuta miguu yake kwa nywele zake; nyumha ikajaa harufu ya yale marhamu.


Ninyi mwaniita Mwalimu, na Bwana; na mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.


Bassi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa ninyi nanyi kutawadhana miguu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo