Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 10:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Awatoapo nje kondoo zilizo zake, huwatangulia; na kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Baada ya kuwatoa wote nje, yeye hutangulia mbele yao na kondoo humfuata, kwa kuwa wanaijua sauti yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake.

Tazama sura Nakili




Yohana 10:4
23 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.


Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata;


Bawabu humfungulia huyu, na kondoo humsikia sauti yake, nae huwaita kondoo zake kwa majina yao, huwapeleka nje.


Mgeni hawatamfuata kabisa, hali watamkimbia, kwa maana hawaijui sauti ya wageni.


wote walionitangulia ni wezi na wanyangʼanyi: lakini kondoo hawakuwasikia.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Kwa kuwa nimewapeni mfano illi hayo niliyowatendea ninyi, na ninyi mtende yayo hayo.


Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.


Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


MWE wafuasi wangu kama mimi nilivyo mfuasi wa Kristo.


BASSI mwe wafuasi wa Mungu, kama watoto wanaopendwa;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.


Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;


BASSI kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake kwa ajili yenu, ninyi nanyi jivikeni nia ile ile kama silaha; kwa maana yeye allyeteswa katika mwili, ameachana na dhambi;


wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya mfano kwa lile kundi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo