Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 10:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 lakini Isa akawaambia, “Nimewaonesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni kwa ipi kati ya hiyo miujiza mnataka kunipiga mawe?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 lakini Isa akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?”

Tazama sura Nakili




Yohana 10:32
16 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Yesu akawajibu, Naliwaambieni, nanyi hamwamini; kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu, ndizo zinazonishuhudia.


Bassi Wayahudi wakaokota mawe tena, illi wampige.


Wayahudi wakamjibu wakinena, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi mawe, bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe, uliye mwana Adamu, wajifanya nafsi yako u Mungu.


Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;


Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


si kama Kain alivyokuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Nae alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake ya haki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo