Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:45 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

45 Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 Naye Filipo akamkuta Nathanaeli, akamwambia, “Tumemwona yule ambaye Mose aliandika juu yake katika kitabu cha sheria, na ambaye manabii waliandika habari zake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu, kutoka Nazareti.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 Naye Filipo akamkuta Nathanaeli, akamwambia, “Tumemwona yule ambaye Mose aliandika juu yake katika kitabu cha sheria, na ambaye manabii waliandika habari zake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu, kutoka Nazareti.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 Naye Filipo akamkuta Nathanaeli, akamwambia, “Tumemwona yule ambaye Mose aliandika juu yake katika kitabu cha sheria, na ambaye manabii waliandika habari zake, yaani Yesu Mwana wa Yosefu, kutoka Nazareti.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika Torati, na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani Isa Al-Nasiri, mwana wa Yusufu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika Torati na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Isa Al-Nasiri, mwana wa Yusufu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 1:45
41 Marejeleo ya Msalaba  

Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo;


Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda?


akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo.


Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.


akamtazama, akasema, Wewe nawe ulikuwa pamoja na yule Mnazareti, Yesu.


Huyu si yule sermala, mwana wa Mariamu, na ndugu wii Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simon? na ndugu zake wanawake hawapo hapa petu? Wakachukizwa nae.


Wakamweleza, Yesu wa Nazareti anapita.


Na Yusuf nae akaondoka Galilaya kutoka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yahudi hatta mji wa Daud, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye wa nyumba na jamaa ya Daud,


Nao walipomwona wakashangaa sana; mama yake akamwambia, Mwanangu, kwani ukatutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Nae Yesu mwenyewe alipokuwa akianza kufundisha, umri wake amekuwa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa mwana wa Yusuf, wa Eli,


Wakamshuhudia wote, wakayastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake: wakanena, Huyu siye Mwana wa Yusuf?


Nae Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mtu wa mji wa Andrea na Petro.


Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu.


Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, yatutosha.


Yesu akawaambia, Mimi ndiye. Yuda nae aliyemsaiiti alikuwa akisimama pamoja nao.


Bassi akawauliza marra ya pili, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.


Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.


Simon Petro, na Tomaso aitwae Didumo, na Nathanael wa Kana wa Galilaya, na wana wa Zebedayo, na watu wengine wawili katika wanafunzi wake, walikuwa mahali pamoja.


Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?


Bassi Yesu alipoinua macho yake akaona makutano mengi yanakuja kwake, akamwambia Filipo, Tununue wapi mikate, hawa wapate kula?


Filipo akamjibu, Mikate ya dinari miateen haiwatoshi, killa mmoja apate kidogo tu.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Nikajibu Wewe nani Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambae wewe unaniudhi.


Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti;


Petro akanena, Fedha sina, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Mnazareti, simama uende.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo