Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:44 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

44 Nae Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mtu wa mji wa Andrea na Petro.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa akina Andrea na Petro.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa akina Andrea na Petro.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

44 Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa akina Andrea na Petro.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

44 Filipo alikuwa raia wa Bethsaida, mji walikotoka Andrea na Petro.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

44 Basi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:44
18 Marejeleo ya Msalaba  

Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo;


Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu.


na Andrea, na Filipo, na Bartolomayo, na Mattayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thaddayo na Simon Mkanani,


Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.


Wakalika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.


Ole wako, Korazin! Ole wako Bethsaida! kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingalifanyika katika Turo na Sodom, wangalitubu zamani, wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.


Simon ambae alimpa jina la pili Petro, na Andrea, ndugu yake; Yakobo na Yohana, Filipo na Bartholomayo.


Wale mitume waliporudi wakamweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda zake kwa faragha mahali pasipo watu, karibu na mji uitwao Bethsaida.


Siku ya pili yake Yesu akataka kuondoka kwenda Galilaya, akamwona Filipo, akamwambia, Nifuate.


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti


Nathanaeli akamwambia, Chaweza kitu chema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.


Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunijua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini, nalikuona.


Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu.


Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kiisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.


Bassi Yesu alipoinua macho yake akaona makutano mengi yanakuja kwake, akamwambia Filipo, Tununue wapi mikate, hawa wapate kula?


Filipo akamjibu, Mikate ya dinari miateen haiwatoshi, killa mmoja apate kidogo tu.


Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo