Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:43 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

43 Siku ya pili yake Yesu akataka kuondoka kwenda Galilaya, akamwona Filipo, akamwambia, Nifuate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Basi, akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Basi, akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Kesho yake Yesu aliamua kwenda Galilaya. Basi, akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Siku iliyofuata Isa aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Siku iliyofuata Isa aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili




Yohana 1:43
19 Marejeleo ya Msalaba  

Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo;


Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, akaenda zake hatta Galilaya;


Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.


Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.


Haya yalifanyika Bethania ngʼambu ya Yardani, alikokuwako Yohana akibatiza.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama na wawili katika wanafunzi wake.


Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yesu akageuka, akawaona wakifuata: akawaambia, Mnatafuta nini?


Nae Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mtu wa mji wa Andrea na Petro.


Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu.


Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, yatutosha.


Mwanzo huu wa ishara Yesu alifanya Kana ya Galilaya, akauonyesha utukufu wake, wanafunzi wake wakamwamini.


Bassi Yesu alipoinua macho yake akaona makutano mengi yanakuja kwake, akamwambia Filipo, Tununue wapi mikate, hawa wapate kula?


Filipo akamjibu, Mikate ya dinari miateen haiwatoshi, killa mmoja apate kidogo tu.


Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali nafuatafuata illi nilishike lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.


Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo