Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ndani yake kulikuwa na uzima, nao huo uzima ulikuwa nuru ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:4
30 Marejeleo ya Msalaba  

Watu waliokaa gizani Waliona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika inchi na kivuli cha mauti, Mwanga umewazukia.


Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Yesu akamwambia, Mimi ni ufufuo na uzima; aniaminiye mimi, ijapo afe, atakuwa ataishi,


Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, watu wakapenda giza zaidi ya nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.


Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao.


Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake;


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Maadam nipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.


ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa.


Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha.


Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza.


Kristo atakapoonekana, aliye uzima wetu, ndipo na ninyi mtaonekana pamoja nae katika utukufu.


ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima,


(na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);


Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwana wake.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo