Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:38 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

38 Wakamwambia, Rabbi (tafsiri yake, Mwalimu), unakaa wapi? Akawaambia, Njoni muone.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Basi, Yesu aligeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata, akawauliza, “Mnatafuta nini?” Nao wakamjibu, “Rabi, (yaani Mwalimu), unakaa wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Basi, Yesu aligeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata, akawauliza, “Mnatafuta nini?” Nao wakamjibu, “Rabi, (yaani Mwalimu), unakaa wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Basi, Yesu aligeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata, akawauliza, “Mnatafuta nini?” Nao wakamjibu, “Rabi, (yaani Mwalimu), unakaa wapi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Isa akageuka, akawaona wakimfuata, akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Mwalimu, unaishi wapi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Isa akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Mwalimu, unaishi wapi?”

Tazama sura Nakili




Yohana 1:38
30 Marejeleo ya Msalaba  

Nae alikuwa na ndugu mwanamke aitwae Mariamu, nae alikuwa ameketi miguuni pa Yesu, akasikia maneno yake.


Bassi makutano mengi wakafuatana nae; akageuka akawaambia,


Akaondoka, akaenda kwa baba yake. Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona, akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni, akambusu sana.


Na Yesu, alipofika mahali pale, akatazama juu, akamwona, akamwambia, Zakkayo, shuka upesi; maana leo imenipasa kushinda nyumbani mwako.


Bwana akageuka, akamtazamisha Petro: Petro akalikumbuka neno la Bwana, jinsi alivyomwambia, Kabla hajawika jogoo leo, utanikana marra tatu.


Na yule mtu aliyetokwa na pepo akamsihi awe pamoja nae: lakini Yesu akamwaga, akisema,


Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yesu akageuka, akawaona wakifuata: akawaambia, Mnatafuta nini?


Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Ilikuwa karibu na saa kumi.


Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabbi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israeli.


Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu.


Bassi Yesu, akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Mnamtafuta nani? Wakamjibu, Yesu Mnazareti.


Bassi akawauliza marra ya pili, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabbi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ngʼambu ya Yardani, uliyemshuhudia wewe, huyu nae anabatiza, na watu wote wanamwendea.


Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabbi, ule.


Hatta walipomwona ngʼambu ya bahari, wakamwambia, Rabbi, umekuja lini hapa?


Petro akawashukia wale watu waliotumwa kwake na Kornelio, akanena, Mimi ndiye mnaemtaka. Mmekuja kwa sababu gani?


Kwa sababu hiyo naiikuja nilipoitwa nisikatae; hassi nauliza, ni neno gani mliloniitia?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo