Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Yohana akawajibu akanena, Mimi nabatiza kwa maji: kati mwenu amesimama msiyemjua ninyi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Yohane akawajibu, “Mimi nabatiza kwa maji, lakini yuko mmoja kati yenu, msiyemjua bado.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Yohane akawajibu, “Mimi nabatiza kwa maji, lakini yuko mmoja kati yenu, msiyemjua bado.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Yohane akawajibu, “Mimi nabatiza kwa maji, lakini yuko mmoja kati yenu, msiyemjua bado.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Yahya akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini kati yenu yupo mtu msiyemjua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Yahya akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:26
14 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Mimi naliwabatizeni kwa maji; bali yeye atawabalizeni kwa Roho Mtakatifu.


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Na hayo watawatendeni kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Bassi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngaliuijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.


Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu.


FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo