Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu kamwe. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu kamwe. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu kamwe. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba, ndiye ambaye amemdhihirisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:18
41 Marejeleo ya Msalaba  

Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Akawagenkia wanafunzi wake akasema, Nimekahidhiwa vyote na Baba yangu: wala hapana mtu ajuae khabari za Mwana illa Baba: wala khabari za Baha illa Mwana, na mtu ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Maneno hayo aliyasema Isaya alipouona utukufu wake, akataja khabari zake.


Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.


Yesu akamwambia, Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba?


Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao.


Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.


Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali.


Si kwamba mtu amemwona Baba, illa yeye atokae kwa Mungu huyu ndiye aliyemwona Baba.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo