Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kutokana na ukamilifu wake sisi sote tumepokea neema kupita neema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kutokana na ukamilifu wake sisi sote tumepokea neema kupita neema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kutokana na ukamilifu wake sisi sote tumepokea neema kupita neema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:16
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ye yote aliye na mali atapewa, na hado atazidishiwa tele: lakini ye yote asiye nayo, hatta ile aliyo nayo ataondolewa.


Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Lakini Yohana alikuwa akimzuia, akinena, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu?


Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


lililo mwili wake, ukamilifu wake akamilishae vitu vyote katika vyote.


na kimjua upendo wake Kristo, ambao hauwezi kufahamiwa vema kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.


Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae,


ambae ndani yake zimo hazina zote za hekima na maarifa, zimesetirika.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo