Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 1:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Alikuwako ulimwenguni, ulimwengu umepata kuwa kwa veye, wala ulimwengu haukumtambua.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Huyo Neno alikuwako ulimwenguni, na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua.

Tazama sura Nakili




Yohana 1:10
23 Marejeleo ya Msalaba  

Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Alikuja kwake, nao walio wake hawakumpokea.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Vyote vyalifanyika kwa huyu. Wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


nayo nuru yangʼaa gizani, wala giza halikuiweza.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


Yesu akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hatta sasa, nami ninatenda kazi.


Illakini hakujiacha hana shahidi kwa kuwa alitenda mema akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwajaza mioyo yenu chakula na furaha.


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;


illakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu, aliye Baba, ambae vitu vyote vimetokana nae, na sisi twarejea kwake; na yuko Bwana mmoja Yesu Kristo, ambae kwa sabiki yake vitu vyote vimekuwa, na sisi kwa sabiki yake.


Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,


Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hatta vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.


FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo